Wednesday, March 29, 2017

Zitto: NECTA Limesema hawana rekodi ya Albert Bashite wala Paul Makonda



Tumejulishwa kwenye Kamati kuwa NECTA hawana rekodi ya Albert Bashite wala Paul Makonda.

Yani wote hawapo kwenye kanzidata ya Baraza la Mitihani. Kwamba Tanzania haijawahi kuwa na wanafunzi wenye majina hayo

Tuesday, March 28, 2017

ANGALIA PICHA JINSI AMBAVYO DSS VIDEO PRODUCTION ILIVYOPOKELEWA MWELA


 NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
DSS TV ilishuhudia umati mkubwa wa watu huko Mwela Mbeya Vijijini pale ambapo DSS VIDEO PRODUCTION walikuwa wakifanya kazi.



WATOTO NAO WALIPATA NAFASI YA KUJIFUNZA KUSHUTI 
















Saturday, March 25, 2017

DSS TV ILITEMBELEA WAFANYAKAZI WA DSS VIDEO PRODUCTION WAKISHUTI KWAYA HUKO MWELA MBEYA VIJIJINI

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
 DSS TV inakuletea picha mbalimbali kutoka Mwela Mbeya ilipotembelea zoezi la kushuti kwaya kutoka kanisa Calvary Assemblies of God.















Friday, March 24, 2017

MATATIZO YANAYOWAPATA WATUMIAJI WA BARABARA YA ISYONJE,KIKONDO NA MAKETE

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Watumiaji wa barabara ya kutoka Isyonje,Kikondo na Makete wakitokea Uyole Mbeya wamekuwa wakikumbana na matatizo mengi ikiwemo kuchelewa kufika wanakokwenda.
DSS TV imeshuhudia abiria kadhaa wakikaa njiani kwa muda mrefu kutoakana na ubaovu wa barabara.

 MAGARI YAKIPISHANA KWA TABU
 BASI LIKIWA LIMEKWAMA HUKU ABIRIA WAKISUBIRI







Saturday, March 11, 2017

KATIBU MKUU ACT_WAZALENDO AHAMIA CHADEMA

       NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,

     Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO jimbo la Tunduma ndugu Joshua Kayange amekihama chama chake na kujiunga na CHADEMA.
     Kayange ambaye alikuwa pia ni mgombea udiwani kata ya  Chipaka iliyopo Tunduma amepokelewa kwenye kikao cha Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) kilichokuwa kikiongozwa na mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Tunduma mheshimiwa Ayubu Sikagonamo ambaye pia ni diwani wa kata ya Chipaka kilichofanyika ukumbi wa Honey Moon uliopo Sogea mjini Tunduma                        Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama ya CHADEMA bwana Kayange amesema hakuna mtu aliyemshawishi kuhamia CHADEMA ila ni kwa  utashi wake mwenyewe."Nimeamua mwenyewe kuhamia CHADEMA hakuna mtu yeyote aliyenishwishi ila ni kwa utashi wangu mwenyewe.Nimeona kule(ACT) nilikuwa napoteza muda kusongesha gurudumu la maendeleo ya Taifa letu."Amesema Kayange.

.
         

Tuesday, March 7, 2017

TANZIA:KATIBU MWENEZI CCM KATA YA MAPOROMOKO AFARIKI DUNIA


Image may contain: one or more people and people sitting

Adam Nsige enzi za uhai wake
NA KENNEDY SIMUMBA
          Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Maporomoko iliyopo ndani ya halmashauri ya mji wa Tunduma ndugu Adam Elia Nsige amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
          Akizungumza na DSS TV katibu wa siasa na uenezi CCM  Momba ndugu Hassan Nyalile amesema  Adam amefariki ikwa ni wiki moja tangu arudi safarini nchini Zambia na msiba upo nyumbani kwa baba yake, mzee Nsige. Mwli wa marehemu Adam Nsige utazikwa leo Jumatano saa sita mchana.

          DSS TV inawapa pole wanafamilia wote wa Adam Nsige na Mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.Mbele yake nyuma yetu.


TANZIA: Mama Kikwete Afariki Dunia


Kupitia ukurasa Instagram wa Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete ameandika ujumbe Kuhusu kifo cha Bi Nuru kama unavyosomeka hapo chini...

"TANZIA Ndugu na Marafiki nasikitika kuwatangazia Msiba/Kifo cha Bibi Yetu Bi.Nuru Khalfan Kikwete Kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana . Innallilllah wainnaillah rajuun.#"


Saturday, March 4, 2017

CHINA,MWAKAJOKA WAWEKANA SAWA,,

             

CHINA,MWAKAJOKA WAWEKANA SAWA,,
Baada ya Kuwepo kwa tofauti ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )
kati ya mbunge wa jimbo la Tunduma mhemiwa Frank Mwakajoka (CHADEMA) na mwenyekiti
wa CHADEMA mkoa wa Mbeya mheshimiwa China leo wamefanya maridhiano kwenye kikao
cha ndani kilichofanyika kwenye ukumbi wa stapples mjini Tunduma mbele ya mh EMMANUEL G MASONGA ambae ni katibu mkuu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini. Viongozi hao
wameombana radhi na kusameheana na kusema sasa wataendelea na harakati za chama kama
kawaida





                                           DSS TV ULIPO TUPO

Friday, March 3, 2017

DSS TV LAU PHONE AND ACCESSORIES

Godbless Lema Aachiwa kwa Dhamana


Breaking: Baada ya kukaa mahabusu kwa miezi minne, Mahakama Kuu Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema (CHADEMA)

Viongozi wa Chadema watinga mahakamani Kusikiliza kesi ya Lema


Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless  Lema akishuka kwenye gari kuingia mahakamani.

 Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakamani  kusikiliza uamuzi wa Mahakama kuhusu dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema unaotolewa leo

Thursday, March 2, 2017

Waziri aonya wasimamizi wa misitu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameonya tabia ya wasimamizi wa misitu kuingia mikataba binafsi na wamiliki wa mifugo hasa ng'ombe kulisha katika hifadhi za misitu nchini.

Amesema kitendo hicho kimesababisha kuharibika kwa uoto wa asili na kuleta uharibifu mkubwa katika hifadhi za misitu.

Akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu nchini (TFS) mjini Dodoma, Profesa Maghembe amesema misitu nchini ipo hatarini kutoweka kutokana na uamuzi binafsi unaofanywa na watu wenye dhamana ya kutunza misitu.

Amesema wanyama wanaoingizwa ndani ya misitu wakiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo wanavuruga utaratibu wa asili na kuua vyanzo vya maji, hivyo kuleta ukame.

Waziri Maghembe amesema hifadhi ya misitu mingi kwa sasa imekuwa ni kama shamba la bibi kutokana na kila mtu kuamua kuitumia kwa shughuli zake binafsi ikiwamo ukataji magogo, utengenezaji wa mkaa na kuingiza mifugo.

Amesema anachukizwa kwa kuteketea kwa misitu huku maofisa wasimamizi wapo na wao wakibaki kuwa sehemu ya malalamiko.

Amesema japokuwa kuna matatizo ya wakala wa misitu ikiwamo ya upungufu wa vitendea kazi pamoja na masuala ya utawala huku wakiwa na wajibu wa kutunza rasilimali za misitu, kasi ya uharibifu wa misitu ni lazima isimamishwe.

Mbowe na Mkewe mikononi mwa TRA, Yawashutumu kwa Makosa haya



Mahakama ya wilaya ya Ilala imewaita mahakamani Freeman Mbowe na mkewe pamoja na aliyekuwa meneja wa klabu ya Bilicanas, Steven Miligo kwa maombi ya mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) baada ya kushindwa kuwapata kwa kutumia barua za wito.

TRA inawashutumu kwa kushindwa kutumia mashine za EFD kutoa risiti, kutoa nyaraka za uongo kwa TRA na kushindwa kutekeleza matakwa ya usimamizi wa kodi.