Wednesday, October 5, 2016

MWAKAJOKA AKOSOA UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Mbunge wa jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA Mheshimiwa Frank George Mwakajoka amesema maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr.John Jombe Magufuli hayafuati matakwa ya wadau kitu ambacho kinapelekea taifa kutopata mapato makubwa.Akitolea mfano wa kampuni moja inayosafirisha  shaba  kutoka bandari ya Dar Es Salaam kupitia Tunduma mpaka sasa haifanyi kazi kwa sababu ya ushuru kuwa mkubwa.Ameyasema hayo leo akiwa kwenye ziara  jimboni kwake kata za Mpemba na Katete.Kwenye ziara hiyo aliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo meya wa mji wa Tunduma mheshimiwa Ally Mwafongo na makamu Meya wa mji Mheshimiwa Herode Jivava.
Pia amedai kuwa Rais Magufuli amempigia magoti Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Joseph Laurent Kabila wafanyabiashara warudi.
Aidha mheshimiwa Mwakajoka ameongeza kuwa utumbuaji majipu wa watumishi wa serikali umekuwa ukifanywa pasipo uchunguzi wa kina."Sisi tumesema hatuna tatizo na utumbuaji majipu kwa watumishi wabovu,lakini uchunguzi wa kina ufanyike kwa mtumishi kabla ya kutumbuliwa"
 Akizungumza kuhusu swala la upasuaji wa barabara ameasema kuwa mpaka sasa kuna barabar mpya kabisa 41 ndani ya halmashauri ya mji wa Tunduma.
KWA HABARI ZAIDI YA VIDEO USIKOSE YOUTUBE DSS TV TUNDUMA TZ,FACEBOOK PAGE DSS Tv na www.sadikitv.blogspot.com
 WANANCHI WAKIFURAHIA KUTEMBELEWA NA MBUNGE WAO NA KUKUMBUSHIA ISHARA YA NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)
 MHESHIMIWA FRANK GEORGE MWAKAJOKA
 DIWANI WA KATA YA MPEMBA
 MAKAMU MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.HERODE JIVAVA(KUSHOTO) NA KATIBU WA MBUNGE MH.HOSEA KIBWANA(KULIA)

 WANANCHI WA KATA ZA MPEMBA NA KATETE WAKIFUATILIA HOTUBA YA MBUNGE WAO
 MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.ALLY MWAFONGO
PICHA KWA HISANI YA DSS MEDIA

No comments:

Post a Comment