Friday, September 30, 2016

TABIRI MATOKEO MECHI YA WATANI WA JADI KESHO

Image result for simba na yanga katika picha

DSS TV HABARI PICHA:MSANII MAARUFU WA ZAMBIA "UJ" AKIWA ANASHUTI WIMBO WAKE WAKE "PIMISHA" FT:CHESTER KUTOKA LUSAKA ZAMBIA

NA KENNEDY SIMUMBA, DSS TV NEWS ROOM
 UJ ALIYEKIFUA WAZI WA KWANZA KUTOKA KUSHOTO NA WA MWISHO KUTOKA KULIA NI MUONGOZAJI WA VIDEO KUTOKA DSS MEDIA ISMAIL ISSA
 WANENGUAJI WA MSANII UJ WAKIWA NA MTANGAZAJI WA DSS TV BANTU MAN
 MTANGAZAJI WA DSS TV,BANTU MAN AKIBADILISHANA MAWAZO NA MSHIRIKA MKUBWA WA MSANII UJ
PICHA YA PAMOJA YA WATU WOTE WALIOKUWA KWENYE ENEO LA KUSHUTIA MKANDA(LOCATION)

Tuesday, September 27, 2016

BREAKING NEWS:LIPUMBA AVULIWA UANACHAMA CUF

 Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kwa kutumia uwezo wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c) limemfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba.

Sunday, September 25, 2016

MABOMU YAPIGWA KWENYE MECHI YA FAINALI YA MBUNGE CUP 2016 TUNDUMA

  • Mchezo wa fainali  kombe la Mbunge Jimbo la Tunduma 2016 kati ya Morning Star na Migmbani FC uliochezwa uwanja wa Shule ya msingi TUNDUMA jioni hii umeingia dosari baada ya mashabiki wanaodaiwa kuwa  ni Migombani FC kuuvamia uwanja.Sintofahamu hiyo imetokea baada ya mlinda mlango wa Morning star kupoteza muda ilihali Morning Star wakiwa wanaongoza mabao 2_1.Kwenye vurugu hizo vitu mbalimbali vimeharibika vikiwemo viti vya wasimamizi wa mechi na vifaa vya DSS TV.





 


 VITI VYA WASIMAMIZI WA MECHI VILIVYOVUNJWA NA MASHABIKI

KINASA SAUTI CHA DSS TV KIKIWA KIMEVUNJWA NA MASHABIKI
POLISI WAKIPIGA MABOMU

MLINDA MLANGO WA MORNING STAR ALIYEDAIWA KUPOTEZA MUDA

Wednesday, September 21, 2016

CHELSEA YAITWANGA LEICESTER 4-2 KOMBE LA EFL, FABREGAS AKITAKATA



Leicester 4-4-2: Zieler 6; Simpson 5, Wasilewski 4.5, Morgan 6, Chilwell 6.5; Schlupp 6, King 7, Drinkwater 7, Gray 6 (Amartey 90); Okazaki 7.5 (Ulloa 75, 6), Musa 6 (Vardy 76, 5) 
Subs not used: Hamer, Benalouane, Kapustka, Mahrez
Booked: Wasilewski, Drinkwater, Chilwell
Sent off: Wasilewski
Manager: Claudio Ranieri 6


Chelsea 4-2-3-1: Begovic 6; Azpilicueta 6, Cahill 5, Luiz 6, Alonso 5; Fabregas 8, Matic 6; Moses 5, Loftus-Cheek 5 (Costa 67, 6.5), Pedro 6 (Hazard 89, 7); Batshuayi 5.5 (Chalobah 80).
Subs: Courtois, Aina, Kante, Willian
Booked: Matic, Luiz
Manager: Antonio Conte 7
Man of the match: Cesc Fabregas
Referee: Bobby Madley 5
Attendance: 29,899 




Monday, September 19, 2016

ZIJUE DALILI ZA MWANAMKE ANAYETOKA NJE YA NDOA

...................


Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume.

Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.

Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:

1.KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

2.KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.

Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.

3.UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4.KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.

Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.

5.KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki.

Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

6.KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.

7.KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake.

Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.

8.KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana.

Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe

PASTOR AWAONYA WANASIASA NA MANABII

Sunday, September 18, 2016

MCHUNGAJI AWATAKA MANABII NA WANASIASA KUMRUDIA MUNGU

MCHUNGAJI WA KANISA LA RESTORATION TUNDUMA
AWATAKA WANASIASA KUACHA TABIA YA KWENDA
KWA WAGANGA WA JADI  KWA MADAI KUWA WANA
LIINGIZA TAIFA LA TANZANIA KWENYE LAANA.
AKIWA ANAHUBIRI IBADA YA ASUBUHI PIA AMETANGAZA
MFUNGO WA MWEZI MZIMA WAMAOMBI NA KAMALIZA KWA KUSEMA
MANABII WA UONGO WA MRUDIE MUNGU KWA KUWA MAOMBI HAYO
YATAKUWA YA KUMWAMBIA MUNGU AWAONDOE KWNYE NAFASI
ZAO ZA UTUMISHI NA UONGOZI WAO.

PASTOR EPHRAIM WA Restoration Bible Church TZ - RBC 
PASTOR Ezekiel Obeid

Friday, September 16, 2016

MAJOGOO WA LIVERPOOL WALIVUNJA DARAJA LA STAMFORD, CHELSEA HOI

Utamu wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ umeendelea kuwa mtamu, hiyo ni baada ya kushuhudia wenyeji wa Daraja la Stamford wakiangukia pua kwa wageni wao ambao ni maarufu kwa jina la Majogoo.

Mabao mawili yaliyofungwa na Dejan Lovren na Jordan Henderson yameifanya Liverpool kupata ushindi dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.





Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha pointi 10 na mabao 11 ya kufunga huku ikiwa imefungwa mabao nane na kulingana pointi na Chelsea na Everton iliyo katika nafasi ya pili.

Lovren aliifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 17 baada ya kupokea pasi ya Philippe Coutinho na bao la pili la timu hiyo lilifungwa dakika ya 36 na nahodha Henderson aliyeuwahi mpira uliookolewa na mabeki wa Chelsea.


Kipindi cha pili Chelsea ilibadilika na kutawala mchezo ambao ilipata bao lake pekee dakika ya 61 kupitia kwa Diego Costa aliyepokea pasi ya Nemanja Matic. Katika mchezo huo beki wa Chelsea, David Luiz alichanika puani na kutibiwa baada ya kugongana na Sadio Mane wa Liverpool.