Saturday, May 13, 2017

MWALIMU TUNDUMA AKAMATWA KWA KOSA LA KUIBA MTOTO HOSPITALI



Mama mmoja mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Songwe na Mwalimu wa Shule ya Msingi Majengo anashililiwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kosa la wizi wa mtoto katika hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa kwa madai kuwa yeye hana uwezo wa kuzaa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Ambwene Mwanyasi amesema kuwa mwanamke huyo amekamatwa Mei 11 mwaka huu saa 11 alfajiri akijaribu kutoroka na mtoto huyo ambaye alikuwa jinsi ya kiume akiwa ni mpacha .
Mwanyasi ameongeza kuwa mama huyo alikuwa amejifunga nguo tumboni ili aonekane mjamzito na mbinu aliyoitumia ni kwenda wodini bila kupitia mapokezi na chanzo cha tukio hilo ni baada ya mwanamke huyo kunyanyaswa na mume wake kwa kutozaa kwa muda mrefu ndipo alipoamua kufanya tukio hilo ili kunusuru ndoa yake isivunjike .
Baadhi ya akina mama hospitalini hapo Atupakisye Gabriel na Wema Kibona wameomba kuimarisha ulinzi hospitalini hapo na kutoruhusu mtu yeyote kuingia wodi hiyo bila kibali kutoka mapokezi ili kunusuru matukio kama hayo.
Wameongeza wanaiomba Serikali kuimalisha ulinzi katika vituo vya afya ikiwa ni pamoja hospitali ya wilaya kuimarisha ulinzi mapokezi ili kuepusha kutokea kwa matukio kama hayo .
Janeth Makoye Mganga Mkuu katika hospitali ya wilaya ya Mbozi amekiri kukamatwa kwa mama huyo katika hospitali hiyo ambapo amesema kuwa mama mwenye mtoto ambaye ana umri wa miaka 17 mkazi wa Kamsamba Momba alikuwa akisubiri kuruhusiwa baada ya kujifungua watoto mapacha wote wakiwa wakiume wakiwa na umri wa siku moja .Hata hivyo alipotoa taarifa ya kutoweka kwa mwanawe mmoja aliwauliza wauguzi ndipo walipofunga milango ili mtu asitoke wala kuingia ndani na alipopekuliwa hakuwa na jalada wala kadi ya kliniki na alipotaakiwa kupimwa ujauzito ndipo alipokutwa na matambara akiwa amejifunga tumboni mithiri ya mimba. Hata hivyo Polisi walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa ambapo atafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.Hili ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo na mkoa wa Songwe kwa ujumla tangu kuanzishwa kwake.Matukio ya wizi wa watoto wachanga mara kadhaa yametokea mkoani Mbeya na baadhi wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha elimu kwa jamii inatakiwa kutolewa hasa kwa wale wasio kuwa na uwezo wa kuzaa ama kutungisha mimba ili kufika katika vituo vya afya na kupima kwani wanawake wamekuwa wakinyanyaswa bila kujua kati ya mama au baba nani ana tatizo la uzazi.

Monday, May 8, 2017

DSS TV YATEMBELEA SHAMBA LA MCHUNGAJI SICHEMBE MPONELA BARAKA INVESTMENT

 NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
DSS TV imetembelea shamba la Mchungaji Obed Sichembe wa kanisa la TAG Bonde la baraka Tunduma.Shamba hilo MPONELA BARAKA INVESTMENT lipo kijiji cha Mponela Chimbuya Mbozi Mkoa mpya wa Songwe ambapo tumejionea shughuli mbalimbali ambazo zinaendelea shambani hapo.USIKOSE KUANGALIA KIPINDI KAMILI YOUTUBE  DSS TV TUNDUMA TZ NA KU_SUBCRIBE ACCUNT YA DSS TV TUNDUMA TZ.
 MCH SICHEMBE AKIWA PEMBENI YA BWAWA LA MAJI
 MESHACK MTAKI(KUSHOTO) AKIMHOJI MCHUNGAJI OBED SICHEMBE