Saturday, March 11, 2017

KATIBU MKUU ACT_WAZALENDO AHAMIA CHADEMA

       NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,

     Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO jimbo la Tunduma ndugu Joshua Kayange amekihama chama chake na kujiunga na CHADEMA.
     Kayange ambaye alikuwa pia ni mgombea udiwani kata ya  Chipaka iliyopo Tunduma amepokelewa kwenye kikao cha Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) kilichokuwa kikiongozwa na mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Tunduma mheshimiwa Ayubu Sikagonamo ambaye pia ni diwani wa kata ya Chipaka kilichofanyika ukumbi wa Honey Moon uliopo Sogea mjini Tunduma                        Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama ya CHADEMA bwana Kayange amesema hakuna mtu aliyemshawishi kuhamia CHADEMA ila ni kwa  utashi wake mwenyewe."Nimeamua mwenyewe kuhamia CHADEMA hakuna mtu yeyote aliyenishwishi ila ni kwa utashi wangu mwenyewe.Nimeona kule(ACT) nilikuwa napoteza muda kusongesha gurudumu la maendeleo ya Taifa letu."Amesema Kayange.

.
         

No comments:

Post a Comment