Monday, February 27, 2017

TIMU YA KINYIKA FC YAPOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI

         Timu ya Kinyika FC imepokea kipigo kikali cha mabao 7-1 kutoka kwa Nungu FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Kinyika kata ya Kinyika wilayani Makete mkoani Njombe,Kipigo hicho kimewaacha hoi mashabiki wa Kinyika FC na kuanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe

 MASHABIKI WAKILAUMIANA

Sunday, February 12, 2017

DIWANI KATA YA MAPOROMOKO AWAPONGEZA WALIMU

      Mheshimiwa diwani wa kata ya Maporomoko iliypo kwenye halmashauri ya mji wa Tunduma mheshimiwa mwalongo amewapongeza walimu wa shule za msingi Maporomoko na Azimio zilizopo kwenye kata yake.
     Tafrija hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Honey Moon Sogea ambapo walimu wa shule hizo walifika kwa wingi.
     Akizungumza kweny tafrija hiyo mheshimiwa Mwalongo amesema viongozi wanapopatwa na tatizo watumie hekima kwani wote ni wamoja na wanafanya kazi kwenye ofisi moja.
aidha mwalongo amesema ataendeleza mikakati yake wliyopanga ya kuwasaidia wanafunzi wa darasa la nne na saba.
                               












MTENDAJI MAPOROMOKO ACHELEWESHA TAFRIJA

     

 MTENDAJI WA KATA YA MAPOROMOKO

    Mtendaji wa kata ya maporomoko alichelewesha tafrija hiyo baada ya kuongoza mgomo wa kutoingia ndani ya ukumbi baada ya mama mmoja kufika kwenye tafrija akiwa amevaa mavazi yenye nembo za CHADEMA.
       Wakizungumzia tukio hilo viongozi mbalimbali walisema kitendo cha mtendaji huyo kuongoza mgomo si kizuri.
       Mtendaji huyo alidai kuwa yeye hawezi kuingia kwenye  tafrija huku  watu wengine wakiwa wamevaa nembo za chama kwani ni kinyume na taaluma aliyoisomea kwa sababu ule si mkutano wa chama bali ni tafrija ya watumishi wa serikali.







Friday, February 10, 2017

RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII



MUDA ULIOWEKWA NI  KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI

JUMAMOSI  Februari,11, 2017


Show last 5 matches and coverageFixtureKick-offStatus
15:30
Arsenal Vs Hull City
18:00
18:00
18:00
18:00
18:00
20:30

JUMAPILI  Februari,12, 2017


Show last 5 matches and coverageFixtureKick-offStatus
16:30
19:00

JUMATATU  Februari,13, 2017



Show last 5 matches and coverageFixtureKick-offStatus
23:00

Saturday, February 4, 2017

RC SONGWE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA CHAKULA



NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Mkuu wa mkoa wa Songwe luteni mstaafu wa jeshi Chiku Galawa amewaomba wananchi wa Tunduma kutunza chakula kilichopo kabla ya msimu mpya wa mavuno.
Mheshimiwa Galawa ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha mapinduzi CCM yaliyofanyika kimkoa mjini Tunduma kwenye uwanja wa ndani wa CCM Tunduma.

ZAMBI AZI PA SHAVU AWAMU ZOTE TANO
Mkuu wa mkoa wa Lindi na mwenyekiti wa CCM Mbeya na Songwe mheshimiwa Godfrey Zambi amezisifia serikali za awamu zote tano tangu Uhuru.
Mheshimiwa Zambi amesema serikali zote tano zimefanya kazi kubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu.
ZAMBI AWAONGOZA VIONGOZI KUPANDA MITI
Kwa upande mwingine zambi amewaongoza viongozi mbalimbali wa chama wilaya na mkoa kwenye zoezi la kupanda miti kwenye shule ya msingi Manga.

SHEREHE ZA MIAKA 40 YA CCM YAVUNA WANACHAMA 40 KUTOKA CHADEMA TUNDUMA

NA KENNNEDY SIMUMBA DSS TV,  
Sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambayo yamefanyika mjini Tuduma kwa mikoa miwili ya kiserikali Mbeya na Songwe.
Maadhimisho hayo yamevuma wanachama takribani 40  kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambao wamepokelewa na mkuu wa mkoa wa Lindi na mwenyekiti wa CCM Mbeya na Songwe mheshimiwa Godfrey Zambi.Kati ya vijana hao 40 wapo pia makamanda(RB) wa CHADEMA wawili kamanda Ally na kamanda Fidodido kama wanavyoonekana pichani hapo juu.
Akizungumzia ujio wa vijana hao katibu wa siasa na uenezi wa CCM Mbeya na Songwe amesema ni mwanzo wa kulirejesha jimbo la Tunduma 2020. 




Friday, February 3, 2017

MVUA YABOMOA NYUMBA 15 TUNDUMA

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri ya mji wa Tunduma imebomoa nyumba 15 kwenye mtaa wa Msamba 2(Kakunku).
Wakizungumza na DSS TV wahanga wa tukio hilo wameiomba serikali iwasaidie kwani  kwa sasa wapo katika hali ngumu.