NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Momba ndugu Hassan Nyalile amesema chama cha mapinduzi wilaya Momba hakitashiriki kwenye maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli yaliyotangazwa na UVCCM Taifa.Akiongea na DSS TV ofisini kwake Nyalile amesema hawafanyi maandamano hayo kwa sababu wanaheshimu na kutii sheria za nchi.
Akizungumzia suala mfuko wa maendeleo ya jamii TASAFU,Nyalile amesema mara nyingi misaada imekuwa ikitolewa sana kwa kufuata itikadi za vyama."Kwa mfano misada badala ya kwenda kwa walengwa wazee wasiojiweza na watu wa makundi maluum imekuwa ikienda kwa vijana wenye nguvu kabisa ambao syo walengwa,Naishauri TASAFU itafute njia nyingine ya kuwafikia walengwa na si hivi ambavyo hali ipo kwa sasa"
Saturday, August 27, 2016
MKUU WA MKOA WA SONGWE ASIMAMIA ZOEZI LA USAFI TUNDUMA
NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni mstaafu Chiku Galawa amesimamia zoezi la kufanya usafi mjini Tunduma kama ilivyo kawaida ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.Akiongea na wananchi mara mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi Luteni huyo mstaafu amesema Tunduma inatakiwa kuwa safi kwa sababu ndiyo kituo cha mataifa yote yaliyokusini mwa bara la Afrika.Lakini pia amewaasa wananchi wa mji wa Tunduma kulinda amani iliyopo na wasikubali kuishi kwenye ajenda za watu wengine.
MKUU WA MKOA WA SONGWE LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA AKIONGEA NA WAKAZI WA TIUNDUMA
DIWANI WA KATA YA MAPOROMOKO MH MWALONGO
WATUMISHI MBALIMBALI WA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA WAKIFANYA USAFI
DIWANI WA TUNDUMA MJINI MH HERODE JIVAVA
GARI LA TAKATAKA LA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA LIKIPELEKA TAKATAKA DAMPO
VIJANA WA SCOUT TUNDUMA NAO WAMESHIRIKI ZOEZI LA USAFI
SCOUT WAKIFANYA USAFI KITUO CHA AFYA MORAVIAN TUNDUMA
KIONGOZI WA SCOUT TUNDUMA MARY KABIGILI
Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni mstaafu Chiku Galawa amesimamia zoezi la kufanya usafi mjini Tunduma kama ilivyo kawaida ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.Akiongea na wananchi mara mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi Luteni huyo mstaafu amesema Tunduma inatakiwa kuwa safi kwa sababu ndiyo kituo cha mataifa yote yaliyokusini mwa bara la Afrika.Lakini pia amewaasa wananchi wa mji wa Tunduma kulinda amani iliyopo na wasikubali kuishi kwenye ajenda za watu wengine.
MKUU WA MKOA WA SONGWE LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA AKIONGEA NA WAKAZI WA TIUNDUMA
DIWANI WA KATA YA MAPOROMOKO MH MWALONGO
WATUMISHI MBALIMBALI WA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA WAKIFANYA USAFI
DIWANI WA TUNDUMA MJINI MH HERODE JIVAVA
GARI LA TAKATAKA LA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA LIKIPELEKA TAKATAKA DAMPO
VIJANA WA SCOUT TUNDUMA NAO WAMESHIRIKI ZOEZI LA USAFI
SCOUT WAKIFANYA USAFI KITUO CHA AFYA MORAVIAN TUNDUMA
KIONGOZI WA SCOUT TUNDUMA MARY KABIGILI
Friday, August 26, 2016
UZINDUZI WA ALBAM MPYA IITWAYO UMEPITA WOTE YA MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA TUNDUMA RBC
SHEKHAINA EPHRAIM
Atazindua albam yake mpya iendayo kwa jina la UMEPITA WOTE itakayofanyika ndani ya kanisa la RESTORATION BIBLE CHURCH RBC TUNDUMA KWA PASTOR EPHRAIM MWAITEBELE tarehe 02.10.2016
NYOTE MNAKARIBISHWA
Atazindua albam yake mpya iendayo kwa jina la UMEPITA WOTE itakayofanyika ndani ya kanisa la RESTORATION BIBLE CHURCH RBC TUNDUMA KWA PASTOR EPHRAIM MWAITEBELE tarehe 02.10.2016
NYOTE MNAKARIBISHWA
RATIBA YA LIGI KUU BARA WEEKEND HII

Jumamosi:
Mbao FC v Mwadui FC (Kirumba) AzamONE saa 10:00 Jioni
JKT Ruvu v Simba SC (Taifa) AzamTWO saa 10:00 Jioni
Azam FC v Majimaji FC Azam (Chamazi) Sports HD 10:00 Jioni
Mbao FC v Mwadui FC (Kirumba) AzamONE saa 10:00 Jioni
JKT Ruvu v Simba SC (Taifa) AzamTWO saa 10:00 Jioni
Azam FC v Majimaji FC Azam (Chamazi) Sports HD 10:00 Jioni
Jumapili:
Yanga SC v African Lyon (Taifa) AzamTWO Saa 10:00 Jioni
Toto African v Mbeya City (Kirumba) azamONE Saa 10:00 Jioni
Yanga SC v African Lyon (Taifa) AzamTWO Saa 10:00 Jioni
Toto African v Mbeya City (Kirumba) azamONE Saa 10:00 Jioni
BREAKING NEWS..MAJAMBAZI YALIYOUWA MAASKARI DAR YAKAMATWA

Majambazi yanayodhaniwa kuua askari huko Mbande yamekamatwa muda huu maeneo ya Vikindu Pwani
Katika tukio hilo Askari mmoja aneuawa na majambazi 14 yamekamatwa
Indaiwa Wengi kati ya hao majambazi ni askari wastaafu wenye uzoefu mkubwa wa kutumia silaha kali...
Bado kiongozi wa majambazi hajajisalimisha kajificha ndani
MKUTANO WA TICAD KUFANYIKA AFRICA KWA MARA YA KWANZA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Monica Juma (mwenye nguo ya kijani) akifuatiwa na Bw. Takeshi Osuga, Balozi wa TICAD kutoka Japan na Mhe. Cherif Mhamat Zene, Balozi wa Chad, Ethiopia wakiongoza moja ya vika vya Maafisa Waandamizi ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Sita wa TICAD.
Mkutano wa 6 wa Kimataifa kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD VI) unatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Agosti, 2016 Jijini Nairobi, Kenya. Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huu kufanyika nje ya Japan tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.
Mkutano huu wa Sita ambao umetanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi tarehe 24 na 25 Agosti, 2016 utafuatiwa na kikao cha Mawaziri tarehe 26 Agosti, 2016 unatarajiwa kupitisha Azimio la Nairobi ambalo litajikita katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazolikabili Bara la Afrika katika kufikia maendeleo na ustawi.
Changamoto hizo ni pamoja na kuporomoka kwa bei za bidhaa zinazotegemewa na nchi za Afrika katika ustawi wake kama vile mafuta, gesi na madini na hivyo kupelekea kuathirika kwa ukuaji wauchumi katika nchi nyingi za Afrika; kulipuka kwa magojwa kama Ebola na kusababisha vifo vilivyopelekea kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi na kupotea kwa nguvu kazi; na Kuongezeka kwa vitendo vya ugaidi.
Vile vile Mkutano huu umetoa kipaumbele kwa ushiriki wa sekta binafsi hususan wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Japan na Afrika. Hivyo mkutano utatoa fursa kwa taasisi zenye dhamana ya kuvutia uwekezaji, biashara na utalii nchini kutangaza fursa zilizopo kwa kampuni za Japan.
Mkutano huu wa 6 wa TICAD ambao unashirikiana kwa karibu na Kamisheni ya Umoja wa Afrika unalenga kuiwezesha Afrika kujitegemea katika kukua na kufikia maendeleo yaliyokusudiwa ikiwemo utekelezaji wa Agenda 2063 ambayo viongozi wa Afrika walikubaliana wakati wakuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika. Agenda 2063 inalenga kuliunganisha Bara la Afrika katika masuala ya kukuza uchumi; kuhamasisha utawala bora na utawala wa sheria; kuhakikisha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja; kuhakikisha amani na usalama unaimarika na kuiweka Afrika kwenye nafasi ya mchangiaji mkuu wa uchumi duniani.
Mkutano wa kwanza wa TICAD uliofanyika Jijini Tokyo mwaka 1993 ulijikita zaidi katika agenda ya kuongeza misaada kwa nchi za Afrika. Kufuatia mkutano huo misaada ya Japan kwa nchi za Afrika iliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 0.6 mwaka 1993 na kufikia Dola bilioni 0.8 mwaka 1998. Hadi kufikia mwaka 2013 msaada wa Japan (ODA) kwa nchi za Afrika ulifikia Dola za Marekani bilioni 2.8.
Mkutano wa 6 wa TICAD ambao kwa mara ya kwanza katika historia unafanyika Afrika utawezesha majadiliano ya ana kwa ana kati ya Wakuu wa Nchi na Wawakilishi kutoka Sekta binafsi.
Kadhalika, mbali na mwenyeji wa Mkutano huu ambaye ni Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta mkutano utahudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shinzo Abe, Viongozi Wakuu kutoka nchi 54 za Afrika pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa na makundi mbalimbali.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huu utaongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Lukuvi atembelea eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex Pugu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.
Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Mwenyekiti ya Kamati ya malalamiko ya wakazi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) Bw. Deus King΄ung΄alo akisoma risala kwa niaba ya wakazi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.
Thursday, August 25, 2016
Wednesday, August 24, 2016
LOWASA AENDELEA NA VIKAO VYA NDANI ILOLO IRINGA LEO NA KUYASEMA HAYA
Leo nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Sisi,
Miezi michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.
Miezi michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.
CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.
Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi tuendelee kuwa wamoja hivi hivi, tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna nguvu kubwa kama ya Umma.
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.
KUHUSU UKUTA .
Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo ,Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .
Wasuluhishi wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. Mtu mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .
POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutaoambana nao mmoja mmoja, hatutahangaika na jeshi tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . Ni bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.
Tabia za baadhi ya viongozi ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki za kidemokrasia .
Tujitokeze kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu . Tuna chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni.
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI MTUNGI AWAITA MEZANI MBOWE NA MAGUFULI
JAJI FRANCIS MTUNGI MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI
MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ameitisha Baraza la Vyama vya Siasa ili kunusuru mvutano uliojitokeza kati ya Jeshi la Polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Jaji Mtungi amevitaka vyama vya siasa vilivyotangaza kufanya maandamano na mikutano isiyo na tija nchi nzima kuacha, badala yake warudi kwenye meza ya mazungumzo ili kuondoa tofauti zinazojitokeza.
Kauli ya Jaji Mutungi imekuja baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) nao kutangaza maandamano ya amani kwa ajili ya kupongeza utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli, huku Chadema kikiitisha maandamano na mikutano isiyo na kikomo nchi nzima, ambayo imepewa jina la Operesheni Ukuta.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Mutungi alisema kufanyika kwa maandamano na mikutano hiyo, hakuwezi kuondoa changamoto za kisiasa zilizopo, hivyo basi wanapaswa kukaa kwenye meza moja kwa ajili ya kujadili tofauti zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.
“Ninawaomba wale wote wenye lengo la kuitisha maandamano na mikutano ya kisiasa kuacha kwa sababu haiwezi kusaidia kuondoa changamoto zilizopo, bali tunapaswa kukaa kwenye meza moja ya mazungumzo ili tuweze kujadili tofauti hizo na kuzipatia majibu,” alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza kuwa licha ya kuwapo kwa jitihada za viongozi mbalimbali kujadili suala hilo, lakini vyama hivyo vimeonekana bado vikiendelea na misimamo yao ya kuitisha mikutano na maandamano yasiyo na kikomo, jambo ambao linaweza kuleta hofu kwa wananchi.
Jaji Mutungi alisema katika kipindi hiki ambacho wananchi wametulia, hakuna haja ya kuwatia hofu au wasiwasi ili ionekane kuwa nchi ina ombwe kubwa la uongozi, jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma juhudi za kuleta maendeleo.
Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi wanapaswa kuheshimu utawala bora na kuacha kujadili mambo ambayo yanaweza kuvuruga amani, badala yake wanapaswa kuangalia mustakabali wa taifa kwa kufanya kazi na kuleta maendeleo.
“Wananchi wanapaswa kuondoa hofu kuhusiana na migongano ya kisiasa inayojitokeza, kwa sababu hakuna ombwe la uongozi, badala yake wanapaswa kufanya kazi kwa masilahi ya taifa ili waweze kuleta maendeleo,” alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, ameamua kuitisha mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ambalo linashirikisha vyama 22, vikiwamo CCM na Chadema wajadili mambo mbalimbali ikiwamo migongano ya kisiasa, ili waweze kuendesha shughuli zao kistaarabu.
Alisema mkutano huo utafanyika Agosti 29 na 30 mwaka huu ukishirikisha wadau mbalimbali.
Jaji Mutungi alisema kutokana na hali hiyo, Agosti 26 kutakuwa na kikao cha kuratibu mkutano huo ambao anaamini ni muhimu kwa ajili ya kuleta maridhiano baada ya tofauti za kisiasa zilizojitokeza.
“Baraza hili ni forum muhimu ya upatikanaji wa maridhiano ya kisiasa kama kuna tofauti zilizojitokeza, kuliko kuitisha mikutano na maandamano yasiyo na tija ambayo yanaweza kusababisha wananchi kupata hofu,” alisema.
Alisema hakuna jambo lenye ugumu katika suala hilo, kwa sababu migongano iliyopo inajadilika ikiwa ni pamoja na kupitia baadhi ya vifungu vya kisheria kwa ajili ya kufatuta mwafaka.
Akizungumzia suala la Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Mutungi alisema migongano iliyopo kwenye chama hicho anaijua, lakini kwa sasa hawezi kuzungumzia lolote kwa sababu mkutano ujao utashirikisha vyama vyote kikiwamo CUF.
“Mimi ni mlezi wa vyama vya siasa… CUF ni miongoni mwa watoto wangu, najua udhaifu wa vyama vyote kikiwamo CUF hadi ubora wao, hata migongano iliyojitokeza ndani ya chama hicho naijua, lakini kwa sasa nashindwa kuongea lolote kwa sababu tuna mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ambalo litajadili mambo mbalimbali, ikiwamo suala la mgogoro wa CUF,” alisema Jaji Mutungi.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wanachama wa chama hicho kuondoa hofu kwa sababu suala hilo litapatiwa ufumbuzi kwa kuondoa tofauti zilizopo.
Jaji Mutungi aliyesema hayo huku wafuasi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakidai kwenda katika ofisi yake kumweleza mambo mbalimbali, ikiwamo ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria na kumwondoa kiongozi huyo kwenye nafasi yake uliofanywa na wafuasi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika hatua nyingine, Chadema kimesema kimesikia wito wa Jaji Mutungi wa kuitisha mazungumzo ambayo iwapo yatatawaliwa na nia njema na dhamira safi ya kuheshimu Katiba ya nchi, yanaweza kuwa na manufaa kwa Watanzania wote.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, ilisema hatua hiyo inaweza kuleta manufaa kama Jaji Mutungu hataegemea upande wa Serikali.
“Wakati Msajili wa Vyama akitoa kauli ya kuzuia kile anachokiita ‘kutunishiana misuli’, Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali limeingilia vikao vya ndani vya chama na kuzuia visiendelee. Hiyo yote ni kinyume na sheria, taratibu na mamlaka yao.
“Mbali na kuzuia vikao vya ndani, Jeshi la Polisi linashikilia watu mbalimbali, wakiwamo wafuasi, mashabiki, wanachama, viongozi wetu kwa kushiriki vikao hivyo, wakitekeleza wajibu na haki zao za kikatiba na kisheria.
“Wakati tunasubiri meza ya mazungumzo kupitia Baraza la Vyama, tunapenda kusisitiza kuwa Chadema itasimama imara kuhakikisha misingi ya demokrasia na utawala unaozingatia Katiba na sheria unafuatwa,” ilisema taarifa hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)












