Saturday, August 27, 2016

MKUU WA MKOA WA SONGWE ASIMAMIA ZOEZI LA USAFI TUNDUMA

NA KENNEDY SIMUMBA  DSS TV,
Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni mstaafu Chiku Galawa amesimamia zoezi la kufanya usafi mjini Tunduma kama ilivyo kawaida ya Jumamosi  ya kila mwisho wa mwezi.Akiongea na wananchi mara mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi Luteni huyo mstaafu amesema Tunduma inatakiwa kuwa safi kwa sababu ndiyo kituo cha mataifa yote yaliyokusini mwa bara la Afrika.Lakini pia amewaasa wananchi wa mji wa Tunduma kulinda amani iliyopo na wasikubali kuishi kwenye ajenda za watu wengine.
 MKUU WA MKOA WA SONGWE LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA AKIONGEA NA WAKAZI WA TIUNDUMA
 DIWANI WA KATA YA MAPOROMOKO MH MWALONGO
 WATUMISHI MBALIMBALI WA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA WAKIFANYA USAFI
 DIWANI WA TUNDUMA MJINI MH HERODE JIVAVA
 GARI LA TAKATAKA LA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA LIKIPELEKA TAKATAKA DAMPO

 VIJANA WA SCOUT TUNDUMA NAO WAMESHIRIKI ZOEZI LA USAFI
 SCOUT WAKIFANYA USAFI KITUO CHA AFYA MORAVIAN TUNDUMA
 KIONGOZI WA SCOUT TUNDUMA MARY KABIGILI

No comments:

Post a Comment