NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Momba ndugu Hassan Nyalile amesema chama cha mapinduzi wilaya Momba hakitashiriki kwenye maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli yaliyotangazwa na UVCCM Taifa.Akiongea na DSS TV ofisini kwake Nyalile amesema hawafanyi maandamano hayo kwa sababu wanaheshimu na kutii sheria za nchi.
Akizungumzia suala mfuko wa maendeleo ya jamii TASAFU,Nyalile amesema mara nyingi misaada imekuwa ikitolewa sana kwa kufuata itikadi za vyama."Kwa mfano misada badala ya kwenda kwa walengwa wazee wasiojiweza na watu wa makundi maluum imekuwa ikienda kwa vijana wenye nguvu kabisa ambao syo walengwa,Naishauri TASAFU itafute njia nyingine ya kuwafikia walengwa na si hivi ambavyo hali ipo kwa sasa"
No comments:
Post a Comment