Wednesday, October 5, 2016

USIKOSE KUANGALIA KNOCKOUT SHOW KESHO ALHAMISI TUKIWA NA WAKALI P THE BOY RAIS WA WANDALI,4G NA SHABABI

NA BANTU MAN DSS TV,


 P THE BOY RAIS WA WANDALI

4G

SHABABI

MWAKAJOKA AKOSOA UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Mbunge wa jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA Mheshimiwa Frank George Mwakajoka amesema maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr.John Jombe Magufuli hayafuati matakwa ya wadau kitu ambacho kinapelekea taifa kutopata mapato makubwa.Akitolea mfano wa kampuni moja inayosafirisha  shaba  kutoka bandari ya Dar Es Salaam kupitia Tunduma mpaka sasa haifanyi kazi kwa sababu ya ushuru kuwa mkubwa.Ameyasema hayo leo akiwa kwenye ziara  jimboni kwake kata za Mpemba na Katete.Kwenye ziara hiyo aliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo meya wa mji wa Tunduma mheshimiwa Ally Mwafongo na makamu Meya wa mji Mheshimiwa Herode Jivava.
Pia amedai kuwa Rais Magufuli amempigia magoti Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Joseph Laurent Kabila wafanyabiashara warudi.
Aidha mheshimiwa Mwakajoka ameongeza kuwa utumbuaji majipu wa watumishi wa serikali umekuwa ukifanywa pasipo uchunguzi wa kina."Sisi tumesema hatuna tatizo na utumbuaji majipu kwa watumishi wabovu,lakini uchunguzi wa kina ufanyike kwa mtumishi kabla ya kutumbuliwa"
 Akizungumza kuhusu swala la upasuaji wa barabara ameasema kuwa mpaka sasa kuna barabar mpya kabisa 41 ndani ya halmashauri ya mji wa Tunduma.
KWA HABARI ZAIDI YA VIDEO USIKOSE YOUTUBE DSS TV TUNDUMA TZ,FACEBOOK PAGE DSS Tv na www.sadikitv.blogspot.com
 WANANCHI WAKIFURAHIA KUTEMBELEWA NA MBUNGE WAO NA KUKUMBUSHIA ISHARA YA NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)
 MHESHIMIWA FRANK GEORGE MWAKAJOKA
 DIWANI WA KATA YA MPEMBA
 MAKAMU MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.HERODE JIVAVA(KUSHOTO) NA KATIBU WA MBUNGE MH.HOSEA KIBWANA(KULIA)

 WANANCHI WA KATA ZA MPEMBA NA KATETE WAKIFUATILIA HOTUBA YA MBUNGE WAO
 MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.ALLY MWAFONGO
PICHA KWA HISANI YA DSS MEDIA

Tuesday, October 4, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS KABILA WA DRC KWA MAZUNGUMZO RASMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha viongozi kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi ya kinyago cha UMOJA Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuriwa na  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kinyago toka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kinyago toka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye ukumbi wa mkutano na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake katika mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016

RAIS KABILA KUWEKA JIWE LA MSINGI TPA LEO


Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila 

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila leo atapigiwa mizingia 21 na kukagua gwaride rasmi jijini hapa.

Baadaye  atazungumza na Rais John Magufuli na mchana ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA). Baadaye  Rais Kabila atashiriki dhifa ya kitaifa ikulu

Rais Kabila amewasili  jana Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu. Rais Kabila anatarajia pia kuzungumzia masuala ya kisiasa nchini mwake ambapo uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu umesogezwa mbele mpaka mwakani jambo ambalo limeleta sintofahamu kwa wananchi wa Kongo.

Kabila ataondoka siku ya Jumatano kurudi Kinshasa.

Rushwa ya ‘mzungu’ yamfukuzisha kazi polisi


JESHI la Polisi visiwani Zanzibar, limesema litamchukulia hatua za kinidhamu ofisa wake mwenyewe cheo cha Sajenti ambaye alionekana hivi karibuni akipokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni.

Hatua hiyo, imekuja baada ya picha za video kusambaa katika mitandao ya kijamii, zinazomwonyesha askari huyo akipokea fedha ambazo hadi sasa hazijajulikana kiwango chake kutoka kwa raia huyo wa kigeni, ambaye alikuwa na kosa la kutofunga mkanda.

Katika video hiyo, raia huyo anaokana kutoa fedha na kumkabidhi askari huyo huku akiahidi kumsaidia ili asikamatwe mbele ya safari.

Tukio hilo lilitokea eneo la Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ingawa askari huyo alitaja eneo la Mahonda akionyesha nia ovu ya kutenda kosa hilo bila kujijua kama anachukuliwa video.

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame alisema jeshi hilo linampongeza raia huyo wa kigeni kwa kutoa taarifa hiyo.

“Jeshi la polisi linachukua nafasi hii kulaani kosa hili, licha ya kua ni kosa la jinai linalifedhehesha jeshi na kulitia doa kutokana na dhamana kubwa lililokabidhiwa,” alisema.

Alisema kwa mujibu  wa taratibu za jeshi hilo, tayari limeanza uchunguzi mara moja na kwamba litachukua hatua zinazostahili.

Kutokana na hali hiyo, Kamishina Hamdani amewataka wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi kufufua mfumo wa upigaji simu kutumia namba za dharura ambazo ni 111 na 112 ili kuwarahisishia wananchi kutoa taarifa.

Afukuzwa kazi kwa kumuita mke wa Obama sokwe


MICHELLE OBAMA,MKE WA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA

Mwajiriwa katika shule moja jijini Georgia, Atlanta, Jane Wood Allen amefukuzwa kazi baada ya kuandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amefanana na sokwe.

Katika taarifa yake, kiongozi wa shule hiyo alisema ubaguzi wa rangi na unyanyasaji hauwezi kuvumiliwa kwenye shule hiyo.

Msemaji wa shule hiyo, Jennifer Caracciolo alithibtisha kuwa uamuzi wa kumfukuza kazi Allen ulifanywa baada ya uongozi wa shule kuona andiko hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Huyu sokwe ataishije kwenye ulimwengu wa kawaida akishaondoka ikulu, iwapo  matanuzi yake hayalipiwi na serikali.” Aliandika Allen kwenye akaunti yake

Monday, October 3, 2016

MADEREVA BODABODA TUNDUMA WAFANYA KIKAO FLAMINGO HOTEL

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Kikundi cha madereva wa bodaboda Tunduma wamefanya kikao chao kwenye hotel ya Flamingo. Kwenye kikao hicho mada kubwa ilikuwa ni mwenyekiti wao OSWARD PETRO ambaye ameshindwa kusimamia kikundi hicho.
Wakichangia mada hiyo wajumbe wa kikao hicho wamesema mwenyekiti huyo aondolewe mara moja na arudishe pesa zote za kikudi ambazo walizozikusanya kwake .
Jackison Joseph aliye kuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesena bodu itakaa na kumjadili mwenyekiti juu swala la kumvua uongozi.
Kwa upande wake MOSES WEGA amewataka madereva wenzake kuendesha bodaboda kwa mwendo wa polepole ili kuondoa kabisa ajari zizizo za lazima.
Mhazina wa kikundi hicho Sijaona Punte
unte maarufu kama wakala amesema utaratibu wa kuunda katiba na kumtafuta mwana sheria utaanza siku chache zijazo.
KWA HABARI ZAIDI ZA VIDEO USIKOSE KUINGIA DSS TV TUNDUMA TZ, FACEBOOK
PAGE DSS TV NA www.sadikitv.blogspot.com

SIJAONA PUNTE,MHAZINA WA KIKUNDI
MADEREVA BODABODA WAKIRAHIA JAMBO

JOSEPH ANDINGILILE,MAKAMU MWENYEKITI WA KIKUNDI
JACKSON JOSEPH,KATIBU WA KIKUNDI

Saturday, October 1, 2016

ANGALIA PICHA 10 ZA HATARI KWA UDHAMINI WA DSS MEDIA



HATARI 

ASANTE MUNGU 

 DUUH

SASA 

NOMA

JAMANI !


DAAH!

MUNGU WANGU 

MOTO MKUBWA WATEKETEZA MADUKA TUNDUMA

KIKOSI CHA YANGA KINACHIIVAA SIMBA LEO TAIFA

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Simba SC
1. Ali Mustafa
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Juma Mahadhi
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Deusi Kaseke
Akiba
- Deogratius Munishi
- Oscar Joshua
- Andrew Vicent
- Nadir Haroub
- Saimoni Msuva
- Haruna Niyonzima
- Obrey Chirwa

MOTO MKUBWA WATEKETEZA MADUKA TUNDUMA

NA KENNEDY SIMUMBA, DSS TV
Moto mkubwa umeteketeza maduka kadhaa kwenye mtaa wa Polisi mjini Tunduma.Moto huo ulianza kuwaka ,majira ya saa 6 za usiku.
Wakizungumza na DSS TV wakazi wa mtaa huo pamoja na viongozi wa serikali wa halmashauri ya mji wa Tunduma wamesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Meya wa mji wa Tunduma mhesimiwa Ally Mwafongo amewapa pole watu wote waliokumbwa na janga hilo.Lakini pia amewaomba wananchi waendelee kuunga mkono zoezi la upanuzi wa barabara kwani gari la zimamoto lilishindwa kuingia eneo la tukio kuzima moto huo.
Kwa upande wake makamu meya wa halmashauri ya mji wa  Tunduma amelaumu serikali kwa kushindwa kuleta gari la zimamoto mkoa mpya wa Songwe kwani magari yote ya zimamoto yamebaki mkoa Mbeya.
Kwa habari zaidi ya VIDEO ya tukio hilo la moto usikose kuangalia kupitia YOUTUBE DSS TV TUNDUMA TZ,FACEBOOK PAGE DSS Tv na www.sadikitv.blogspot.com
MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.ALLY MWAFONGO AKIZUNGUMZA NA DSS TV
MAKAMU MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.HERODE JIVAVA AKIZUNGUMZA NA DSS TV.
 MTENDAJI WA KATA YA TUNDUMA MH.MOHAMED MWAKALOBO AKIZUNGUMZA NA DSS TV
 MIKA SIMON, MMOJA WA WAHANGA WA JANGA LA MOTO
DINA ALLY MHANGA WA JANGA LA MOTO