NA KENNEDY SIMUMBA, DSS TV
Moto mkubwa umeteketeza maduka kadhaa kwenye mtaa wa Polisi mjini Tunduma.Moto huo ulianza kuwaka ,majira ya saa 6 za usiku.
Wakizungumza na DSS TV wakazi wa mtaa huo pamoja na viongozi wa serikali wa halmashauri ya mji wa Tunduma wamesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Meya wa mji wa Tunduma mhesimiwa Ally Mwafongo amewapa pole watu wote waliokumbwa na janga hilo.Lakini pia amewaomba wananchi waendelee kuunga mkono zoezi la upanuzi wa barabara kwani gari la zimamoto lilishindwa kuingia eneo la tukio kuzima moto huo.
Kwa upande wake makamu meya wa halmashauri ya mji wa Tunduma amelaumu serikali kwa kushindwa kuleta gari la zimamoto mkoa mpya wa Songwe kwani magari yote ya zimamoto yamebaki mkoa Mbeya.
Kwa habari zaidi ya VIDEO ya tukio hilo la moto usikose kuangalia kupitia YOUTUBE DSS TV TUNDUMA TZ,FACEBOOK PAGE DSS Tv na www.sadikitv.blogspot.com
MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.ALLY MWAFONGO AKIZUNGUMZA NA DSS TV
MAKAMU MEYA WA MJI WA TUNDUMA MH.HERODE JIVAVA AKIZUNGUMZA NA DSS TV.
MTENDAJI WA KATA YA TUNDUMA MH.MOHAMED MWAKALOBO AKIZUNGUMZA NA DSS TV
MIKA SIMON, MMOJA WA WAHANGA WA JANGA LA MOTO
DINA ALLY MHANGA WA JANGA LA MOTO
No comments:
Post a Comment