Tuesday, October 4, 2016

Afukuzwa kazi kwa kumuita mke wa Obama sokwe


MICHELLE OBAMA,MKE WA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA

Mwajiriwa katika shule moja jijini Georgia, Atlanta, Jane Wood Allen amefukuzwa kazi baada ya kuandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amefanana na sokwe.

Katika taarifa yake, kiongozi wa shule hiyo alisema ubaguzi wa rangi na unyanyasaji hauwezi kuvumiliwa kwenye shule hiyo.

Msemaji wa shule hiyo, Jennifer Caracciolo alithibtisha kuwa uamuzi wa kumfukuza kazi Allen ulifanywa baada ya uongozi wa shule kuona andiko hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Huyu sokwe ataishije kwenye ulimwengu wa kawaida akishaondoka ikulu, iwapo  matanuzi yake hayalipiwi na serikali.” Aliandika Allen kwenye akaunti yake

No comments:

Post a Comment