Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila
Baadaye atazungumza na Rais John Magufuli na mchana ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA). Baadaye Rais Kabila atashiriki dhifa ya kitaifa ikulu
Rais Kabila amewasili jana Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu. Rais Kabila anatarajia pia kuzungumzia masuala ya kisiasa nchini mwake ambapo uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu umesogezwa mbele mpaka mwakani jambo ambalo limeleta sintofahamu kwa wananchi wa Kongo.
Kabila ataondoka siku ya Jumatano kurudi Kinshasa.
No comments:
Post a Comment