Wednesday, August 31, 2016

DSS TV HABARI Breaking New: CHADEMA imetangaza kusitisha maandamano

Breaking New: CHADEMA imetangaza kusitisha maandamano

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kisitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA.

Akitangaza uamuzi huo, mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa, wamefanya mazungumzo na viongozi mbalimbalia wakiwemo viongozi wa dini, BAKWATA, Baraza la Maaskofu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Jukwaa la Katiba na Jukwaa la wahariri na kuona wana kila sababu ya kusikiliza ushauri huo.

Aidha, maandamano hayo yameahirishwa kwa mwezi mmoja ili kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka 

DSS TV HABARI ANGALIA VIDEO HARABMEE YA WALEMAVU TUNDUMA

WAZIRI ALIYESINZIA MKUTANONI AUAWA KOREA KASIKAZINI

 Rais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-ju

Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.

Waziri huyo wa elimu Kim Yong-jin anadaiwa kusinzia katika mkutano wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Baadhi ya ripoti zinasema waziri huyo, ambaye amekuwa pia akihudumu kama mmoja wa manaibu wa waziri mkuu, alitekwa na usingizi wakati wa mkutano huo jambo ambalo lilichukuliwa kama kumkosea heshima kiongozi huyo.

Maafisa wa Korea Kusini wamesema wanaamini waziri huyo aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Julai.

Serikali hiyo inasema maafisa wengine wawili walilazimishwa kwenda kuishi maeneo ya mashambani, "kupewa upya mafunzo".

Korea Kusini iliwahi kutoa taarifa kwamba kiongozi wa jeshi la Korea Kaskazini Ri Yong-gil alikuwa ameuawa mwezi Februari mwaka huu.

Lakini mwezi Mei mwaka huu, ilibainika kwamba alikuwa bado hai na alikuwa akihudhuria mikutano na hafla rasmi za serikali.

Mara ya mwisho Korea Kaskazini kutangaza hadharani kwamba ilikuwa imemuua afisa mkuu serikalini ilikuwa ni mwaka 2013 wakati mjombake rais wa nchi hiyo, Chang Song-thaek aliuawa mwaka 2013.

Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege.

Gazeti hilo lilisema wawili hao waliuawa mapema mwezi huu.

Watu zaidi ya kumi wameuawa tangu Kim Jong-un achukue hatamu miezi mitano iliyopita.

Baadhi ya wachanganuzi wa masuala ya siasa wanasema huenda kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 32, hutumia njia ya kuwaua watu hadharani kusisitiza udhibiti wake kama kiongozi.
Waziri huyo alichunguzwa baada ya kusinzia mkutano wa Rais Kim Jong-un

Mapema mwezi huu, naibu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Kusini.

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK


SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha 


Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya.

 Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia. 

 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune 
 Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi. 
 Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi . 
 Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi . 
 

KURASA ZA MICHEZO KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 31,2016

BAADA YA VIONGOZI WA JUU CHADEMA KUKAMATWA JUZI LOWASSA ATOA YA MOYONI




Image result for LOWASSA
EDWARD LOWASSA 
Nimelazimika kushika kalamu na kuandika masikitiko yangu,kwa jinsi serikali ya CCM inavyoelekea kulitumbukiza taifa letu katika mkwamo na machafuko ya kisiasa.
Sote tunafahamu hali ya kisiasa ilivyo tete kwa sasa hapa nchini.Serikali inaukandimiza upinzani na demokrasia kwa jumla.Tumelazimika kutangaza operesheni UKUTA kupinga ukandamizaji huo.
Binafsi nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea operesheni hii,pamoja na vitisho vya dola.Siku zote sisi CHADEMA na UKAWA Kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu taifa letu.Maandamano haya ya Sept mosi ni ya amani, lakini vitendo vya jeshi la Polisi vimewapa wasiwasi watanzania.
Nimepokea Simu nyingi sana kutoka kwa viongozi wastaafu na watu wengine mashuhuri na wa heshima kubwa hapa nchini kututaka tuzungumze na serikali ili kuliepusha taifa letu kutumbukia katika machafuko.
Tumeanza juhudi hizo, nyote ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Mzee Mkapa.Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za kuwanyooshea wenzetu mkono wa amani.
Lakini cha kushangaza wenzetu hawako tayari kuupokea mkono huo.Jana(jumatatu) tukiwa katika kikao cha kujadiliana jinsi ya kuunyosha zaidi mkono huo, jeshi la Polisi likaja na kuukata mkono huo kwa kutukamata.
Kitendo kile kwangu binafsi kimezidi kuniimarisha na kunipa nguvu zaidi ya kudai demokrasia na kuheshimu katiba ambayo viongozi wetu waliapa kuifuata na kuitetea.
Edward Ngoyai Lowassa
Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA

Tuesday, August 30, 2016

WALEMAVU WAFANYA HARAMBEE LEO TUNDUMA

Harambee hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa High Class  na kuhudhuriwa na viogozi mbalimbali akiwemo makamu meya wa Tunduma Mheshimiwa Herode Jivava,mwenyikiti wa Unyamwanga na mgeni rasmi alitarajiwa kuwa  mheshimiwa Frank Mwakajoka mbunge wa jimbo la Tunduma ambaye  aliwakilishwa na  mheshimiwa Mwavirenga   diwani wa kata ya Sogea.Mheshimiwa Mwavirenga aliwakabidhi walemavu cheti cha usajiri


  Baba mlezi na Mama mlezi

 Cheti cha usajiri


 Mwenyekiti wa kikundi akikabidhiwa cheti cha usajiri

USIKOSE KUANGALIA VIDEO YA HARAMBEE HIYO KESHO KWENYE 
YOUTUBE YA DSS TV TUNDUMA TZ 





Monday, August 29, 2016

MSEMAJI WA CCM AMSIFU LOWASSA

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,
Msemaji wa chama cha  mapinduzi CCM Christopher Ole Sendeka amesema Lowasa ni muungwana asingekataa kumpa mkono Rais John Magufuli."Namfahamu Lowassa ni muungwana hawezi kuacha kusalimiana kwa kumshika mkono Rais Magufuli.Wamekutana viongozi,Rais na Waziri mkuu mstaafu hawawezi kuacha kusalimiana".Rais Magufuli na Waziri mkuu mstaafu Lowassa walikutana kwenye sherehe ya Jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Rais wa awamu ya tatu mheshimiwa Benjamini William Mkapa iliyofanyika wiki iliyopita.Siku chache zilizopita katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mheshimiwa Dr.Alli Mohamed Shein walipokutana kwenye mazishi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Abudi Jumbe.Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu

YAFAHAMU MATUKIO MAKUBWA MANNE YATAKAYOFANYIKA NCHINI TANZANIA SEPTEMBA MOSI


1.KUPATWA KWA JUA
Tukio la kwanza ni kupatwa kwa jua ambapo tukio hilo litaonekana kwa wakazi wa mikoa ya Mbeya na Njombe.Kwa mjibu wa mamlaka ya utalii nchini wamesema tayari watalii mbalambali 
wameannza kumiminika kwenye mikoa hiyo ili kuweza kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
2.JESHI LA ULINZI KUAZIMISHA MIAKA 52 YA MAJESHI SEPTEMBA 1
Tukio la pili ni jeshi la ulinzi la wananchi la Tanzania JWTZ litaazimisha miaka 52 ya majeshi Septemba Mosi.Kwa mjibu wa msemaji wa JWTZ amesema tayari shamrashamra zimeanza
3.MAANDAMANO YA UKUTA
Tukio la tatu ni Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufanya maandamano ya Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA
Licha ya ktazo kutoka jeshi la polisi nchini lakini bado viongozi wa juu wa chama hicho wameendelea kusisitiza kuwepo kwa maandamano hayo.
 4.WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa atahamia rasmi Dodoma ambapo anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim MajaliwaÂ