EDWARD LOWASSA
Nimelazimika kushika kalamu na kuandika masikitiko yangu,kwa jinsi serikali ya CCM inavyoelekea kulitumbukiza taifa letu katika mkwamo na machafuko ya kisiasa.
Sote tunafahamu hali ya kisiasa ilivyo tete kwa sasa hapa nchini.Serikali inaukandimiza upinzani na demokrasia kwa jumla.Tumelazimika kutangaza operesheni UKUTA kupinga ukandamizaji huo.
Binafsi nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea operesheni hii,pamoja na vitisho vya dola.Siku zote sisi CHADEMA na UKAWA Kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu taifa letu.Maandamano haya ya Sept mosi ni ya amani, lakini vitendo vya jeshi la Polisi vimewapa wasiwasi watanzania.
Nimepokea Simu nyingi sana kutoka kwa viongozi wastaafu na watu wengine mashuhuri na wa heshima kubwa hapa nchini kututaka tuzungumze na serikali ili kuliepusha taifa letu kutumbukia katika machafuko.
Tumeanza juhudi hizo, nyote ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Mzee Mkapa.Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za kuwanyooshea wenzetu mkono wa amani.
Lakini cha kushangaza wenzetu hawako tayari kuupokea mkono huo.Jana(jumatatu) tukiwa katika kikao cha kujadiliana jinsi ya kuunyosha zaidi mkono huo, jeshi la Polisi likaja na kuukata mkono huo kwa kutukamata.
Kitendo kile kwangu binafsi kimezidi kuniimarisha na kunipa nguvu zaidi ya kudai demokrasia na kuheshimu katiba ambayo viongozi wetu waliapa kuifuata na kuitetea.
Edward Ngoyai Lowassa
Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA
Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA
No comments:
Post a Comment