Saturday, January 21, 2017

THOMAS ULIMWENGU APATA ULAJI ULAYA

Ulimwengu ataingia kikosi cha kwanza moja kwa moja na kazi yake kubwa itakuwa ni kuhakikisha timu hiyo inabeba ubingwa wa ligi kuu
Hatimaye mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, amejiunga na klabu ya Athletic Football Club Eskilstuna ya Sweden kwa mkataba wa miaka miwili.
Meneja wa Ulimwengu Jamali Kisongo, ameiambia Goal, timu hiyo imemsajili Ulimwengu kwa mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuanza kuitumikia timu hiyo hivi karibuni.

“Ni kweli tumekamilisha mkataba wa miaka miwili ya klabu ya Athletic Football Club Eskilstuna ,mimi na Ulimwengu tunatarajia kwenda Sweden, kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya mambo ikiwemo vibali vya kufanyia kazi na nyumba ya kuishi,” amesema Kisongo.

Mshambuliaji huyo aliyetamba na TP Mazembe ya DR Congo, amesema timu hiyo kwa muda mrefu ilikuwa ikimfatilia, Ulimwengu na hata baada ya kumaliza mkataba wake ili ilitaka kumsajili lakini ilishindakana kwakua kipindi cha usajili kilikuwa bado hakijafika.

Amesema Athletic Football Club Eskilstuna ni moja kati ya timu kubwa nchini Sweden, hivyo kama ulimwengu atapambana anaweza kufika mbali na kuweza kuonekana na timu kubwa na kuweza kusajiliwa.

“Tunashukuru kwa mpango huo kukamilika nafikiri kilichobaki ni kwa mchezaji mwenye aweze kuonyesha juhudi kwa kupambana ili aweze kujitengenezea mazingira ya kusajiliwa na timu kubwa za ndani na nje ya Sweden,”amesema Kisongo.

Meneja huyo amesema anaimani kubwa na mteja wake, kuwa hatomuangusha kama ilivyo kwa Mbwana Samatta, ambaye anatamba na KRC Genk ya Ubelgiji.

Amesema Ulimwengu kabla ya kuamua kutua Sweden, alikuwa na ofa nyingi mkononi zinazo mhitaji mchezaji huyo lakini ofa ya Sweden ndiyo ilikuwa yakuvutia zaidi na ndiyo maana wakaamua kuikubali.

Kwamujibu wa Kisongo, Ulimwengu ataingia kikosi cha kwanza moja kwa moja na kazi yake kubwa itakuwa ni kuhakikisha timu hiyo inabeba ubingwa wa ligi kuu ya taifa hilo ambayo inashirikisha timu 16 na inatarajiwa kuanza kutimua vubmi Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment