Saturday, January 21, 2017

MOURINHO:HAKUNA BEKI BORA KAMA VALENCIA


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema haoni beki bora wa kulia zaidi ya Antonio Valencia
Jose Mourinho amesema beki wa Manchester United Antonio Valencia ni beki bora zaidi wa kulia katika mpira wa miguu.
United waliboresha mkataba wa mchezaji huyo kwa kumwongezea mwaka mmoja ili kumfunga klabuni hapo hadi 2018.
Awali alisajiliwa kama winga 2009, Valencia amejiimarisha na kuwa mchezaji muhimu zaidi katika safu ya ulinzi ya Mourinho, akifanikiwa kuanza mechi 23 katika michuano yote.
Na Mourinho amefurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo, ambaye anaamini anayo kila sababu ya kusifiwa kwa mchango wake na alistahili dili jipya.
 “Sidhani amepata dili jipya kama thawabu, silioni jambo hili kwa mtazamo huo,” Mourinho alikiambia MUTV.
“Nadhani ni beki bora zaidi wa kulia kwa sasa. Hakuna beki bora zaidi yake katika soka. Ni haki yetu kumbakisha mchezaji mahiri. Sioni kama ni thawabu, amestahili.
“Ni kipaumbele chetu kuwa na wachezaji bora na mtu mwema kama yeye.
“Antonio anacheza vizuri mno, nadhani. Msimu huu anacheza katika kiwango kikubwa ajabu.”
 “Hakuwa akicheza kama beki wa kulia, mimi nimemtaka kucheza nafasi ya beki wa kulia,”  meneja huyo alieleza jinsi alivyoshindwa kumchukua mchezaji huyo alipokuwa Real Madrid Hispania.
“Lakini Manchester United walikuwa imara na wenye akili. Walizuia kila uwezekano wa kumpoteza.”
Heshima kubwa za Valencia katika Old Trafford ni pamoja na mataji mawili ya Ligi Kuu, mnamo 2011 na 2013, kadhalika Kombe la FA na Medali za Kombe la EFL.

No comments:

Post a Comment