Monday, January 30, 2017

MWENYEKITI CCM MBEYA APIGWA RISASI.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Ephreim Mwaitenda amejeruhiwa kwa risasi baada ya watu wasiojulikana kuvunja dirisha na kuchana nyavu za dirisha katika eneo la shamba lake wilayani Kyela kisha kupenyeza mtutu na kumpata Mwaitenda mgongoni na kusababisha baadhi ya risasi kukwama katika mwili wake eneo la mgongo.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Emmanuel Lukula amesema Mwaitenda alipigwa risasi majira ya saa nane usiku januari 30 mwaka huu kwa risasi za goroli na bunduki iliyotengenezwa kienyeji na majeruhi amekimbizwa hospitali ya Wilaya ya Kyela kabla ya kuhamishiwa rufaa Mbeya . Lukula amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuwabaini wahusika na katika eneo la tukio baadhi ya vitu vimeokotwa vitavyosaidia uchunguzi. Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Zongo Lobe Zongo baada ya kupata taarifa amesema walifanikiwa kumsafirisha majeruhi hadi hospitali ya rufaa Mbeya. Aidha amewapongeza Polisi kwa kufika haraka eneo la tukio na Madaktari ambao wanafanya juhudi za kuondoa risasi zilizokwama mgongoni. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr Godlove Mbwanji amesema wamempokea majeruhi huyo ambapo walimfanyia X-ray na wakati wowote walimfanyia upasuaji kuondoa risasi zilizokwama mgongoni.



No comments:

Post a Comment