NA KENNEDY SIMUMBA,DSS TV
Timu ya Yanga yenye masikani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar Es Salaam jioni ya leo imeshindwa kukwea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya African Lyon.Lyon walikuwa wa kwanza kupata bao lakini mshambuliaji Mrundi Amis Tambwe akaisawazishia Yanga katika mechi iliyochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment