Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli
akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu
Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa
kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
leo Novemba 11, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji
Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel
John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi
huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 11, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es
Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba,
2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini
Ujerumani.
Mwili
wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee
Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili
huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe.
Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu
wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa
Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baada
ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John
Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na
wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye
jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho
Jumamosi huko Urambo.
Wakati huo huo,
Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa
Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya
saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe.
Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali
baada ya kuugua ghafla.
"Nimeshtushwa
sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job
Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge,
Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na
msiba huu.
"Tutamkumbuka
Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi
wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika
tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016
Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna
Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu
Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa
kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
leo Novemba 11, 2016
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama
Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu
Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga
mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
salaam leo Novemba 11, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli
akimpa pole binti wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta
alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 11, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa
pole Mhe. John Sitta, mtoto wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel
John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi
huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo
Novemba 11, 2016
ais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa
pole wanafamilia wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta
alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 11, 2016.
ais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa
pole wanafamilia wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta
alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 11, 2016

katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Nobemba 11, 2016

No comments:
Post a Comment