Mkuu wa wilaya Momba mheshimiwa Juma Ilando amewaongoza wananchi kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Oktoba,17,mwaka 1999 hospitali ya mtakatifu Thomas nchini Uingereza.
Maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika Tunduma kwenye uwanja wa shule ya sekondari Mwalimu JK Nyerere ambapo mkuu wa wilaya Juma Ilando amewahutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mheshimiwa Ilando amesema wananchi wanakiwa kuishi kwa upendo kama ambavyo Baba wa Taifa alivyosema enzi za uhai wake.Lakini pia amewaasa viongozi na wananchi kuto kuchukua au kupotea rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.
Ameongeza kuwa maadhimisho ya kumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere kwa mwaka huu yatakwenda sambamba na usafi ambapo kesho jumamosi mheshimiwa juma ilando atawaongoza wakazi wa Tunduma kwenye zoezi la usafi.
Lakini pia mkuu wa wilaya Momba amewaongoza viongozi wa serikali na viongozi wa dini kupanda miti.
BANGO LA KUWAKARISHA WAGENI WALIOKUWA WAKIWASILI SHULENI
MWANAAFUNZI MAGRETH WESTON WA SHULE YA SEKONDARI MPAKANI
UMATI WA WATU WENGI UMESHUHUDIWA
WANAFUNZI WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOTUBA YA MKUU WA WILAYA
MKUU WA WILAYA AKIELEKEA KUPANDA MTI
MKUU WA WILAYA YA MOMBA JUMA ILANDO AKIPANDA MTI
MAKAMU MWENYEKITI WA MJI HERODE JIVAVA AKIPANDA MTI
MKUU WA WILAYA AKINAWA MIKONO BAADAY KUPANDA MTI
MCHUNGAJI WA KANISA LA AFRICAN, NOEL SIMCHIMBA AKIPANDA MTI
PICHA YA PAMOJA YA VIONGOZI
No comments:
Post a Comment