Monday, January 16, 2017

Hivi ndivyo vipigo vitakatifu alivyowai kupata Pep Gurdiola


Image result for pep guardiola
Pep Gurdiola na yeye ameingia kwenye mfumo wa 4G kama Yanga.Toka Pep aje Uingereza katika ligi kuu ya EPL Everton ndio wamempa kipigo kikubwa zaidi.Ameshafungwa goli 4 na Leicester City huku akipigwa 3 na Chelsea.Hii sio mara ya 1 kwa Pep kula kipigo cha mbwa mwizi,huko alikotoka ameshapigwa pigwa sana.Hizi ni mechi ambazo Pep alifungwa goli nyingi zaidi.

19/10/2016 Barcelona 4 – Man City 0.

Hii ilikuwa mechi ya UEFA katika hatua ya makundi.Pep alikuwa na miezi miwili toka aichukue Man City.Katika hatua za makundi City alikuwa kundi moja na Barcelona.Man City walisafiri kwenda Nou Camp kuwakabili Barcelona,katika mechi hiyo zidi ya timu yake ya zamani Gurdiola alikutana na dhahma hiyo huku Lioneil Messi akipiga hat trick na Neymar akifunga goli moja.

29/4/2014 Bayern Munich 0 – Real Madrid 4.

Hii ilikuwa nusu fainali ya UEFA,huku Bayern wakiwa na goli 1 walilolipata Santiago Bernabeu walihitaji suluhu tu kwenda fainali.Lakini Real Madrid wakiwa na nyota wao Cristiano Ronaldo walimshushia kipigo hicho Pep Gurdiola na kuitupa Bayern nje ya UEFA.Ni Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo walipiga goli mbili kila mmoja na kumtupa nje ya mashindano hayo Pep Gurdiola.

30/1/2015 Wolfburg 4 – Bayern Munich 1.

Kelvin De Bruyne ambae sasa yuko na Gurdiola alifunga mara mbili na Bast Dost alifunga pia mara mbili.Hiki ni kati ya vipigo vikubwa alivyopata akiwa Bundesliga japo pamoja na kipigo ila aliibuka na kombe hilo.

12/4/2014 Bayern Munich 0 – Borrusia Dortmund 3.

Kipigo kingine kwa Gurdiola kilitoka kwa wapinzani wao wakubwa Ujerumani.Borrusia Dortmund waliichapa Bayern Munich ya Gurdiola goli 3 huku mchezaji wa sasa wa Manchester United Henrikh Miktaryan akifunga moja kati ya magoli hayo.Magoli mengine ya Dortmund yaliwekwa kimiani na Marco Reus na Jonas Hoffman.

15/1/2017 Everton 4 – Man City 0

Gurdiola toka ajiunge na Man City hii ni mara ya nne anafungwa goli nne katika mechi moja.Alifungwa na Leicester goli nne kwa mbili,alifungwa na Barcelona goli nne kwa bila na sasa anakufa mbele ya Everton tena goli nne kwa sifuri.Makinda mawili Adeemola Lookman aliyenunuliwa wiki iliyopita akitokea Charton na Tom Davies aliyepandishwa kutoka academy ya vijana walipeleka kilio City wakifunga goli moja moja.Kevin Miralass na Lukaku walitangulia kucheka na nyavu.

No comments:

Post a Comment