Monday, December 19, 2016

NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR CHADEMA ASEMA UMOJA NI NGUVU.

NA NEEMA JUSTIN DSS TV,
MH.SALUM MWALIM, NABU KATIBU MKUU CHADEMA ZANZIBAR.

Naibu katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Salum Mwalim amesema umoja na mshikamano ndani ya chama  ni njia pekee kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza na viongozi wa chama kwenye ukumbi wa Honey Moon mjini Tunduma,Mheshimiwa Mwalim amesema viongozi na wanachama wanatakiwa kufuta kabisa ukabila ndani ya chama ili kujenga msingi utakaokipatia chama ushindi mkubwa mwaka 2020.Amesema wanazunguka Tanzania nzima ili kuimarisha chama na kutoa dozi kwa CCM.
Kwa upande mwingine Mwalim amesema kwa hali ilivyo kwa sasa hata wana CCM wenyewe pamoja na viongozi wao wanatamani UKUTA ukizingatia wanafunzi wa wengi wamenyimwa mkopo wa elimu ya juu.

LOWASA AKOSEKANA
Akizungumza na DSS TV juu ya kutokuwepo kwa waziru mkuu mstaafu na mjumbe wa halmashauri kuu mheshimiwa Edward lowassa amesema alipata udhuru wa kifamilia wakiwa Tabora hivyo akarudi Dar Es Salaam.




No comments:

Post a Comment