MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIWA WAMETULIA KIMYA BAADA YA KUFUNGWA
NA KENNEDY SIMUMBA,CCM SOKOINE MBEYA,
Ibrahim Ajib na Shinza Kichuya wamempa Mnyama heshima yake wakitupia kila moja Simba ikiibuka na ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Mbeya City jioni hii
Simba walionekana kuwa na dalili za kuibuka na ushindi mapema tu baada ya washambulizi wake Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya na Fredrick Blagnon kulisakama lango la Mbeya City mithili ya nyuki.
Iliwachukua dakika sita tu tangu filimbi ya mwamuzi ipulizwe Simba kupata bao kupitia kwa Ibrahim Ajibu ‘Fundi’, ambaye alipiga mpira wa adhabu mujarabu na kutinga moja kwa moja wavuni,
Ajibu aliendelea tena kulikasakama lango la Mbeya City baada ya kuachia shuti kali dakika ya 15 lakini mpira uligonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kuokolewa na walinzi wa Mbeya City.
Simba walipata penati baada ya Blagnon kufanyiwa madhambi na kupiga mwenyewe lakini alikosa baada ya kipa wa Mbeya City kupangua mpira.
Kiungo mshambuliaji wa pembeni wa Simba aliye kwenye kiwango bora kwa sasa, Shiza Kichuya alifunga bao la pili mnamo dakika ya 33 baada ya kumhadaa beki wa Mbeya City na kuupiga mpira kwa ufundi wa hali ya juu na kuandika bao lake la sita msimu huu akiwa ndio kinara wa mabao.
BASI LA MBEYA CITY LIKIWA LINAINGIA UWANJANI
BASI LA SIMBA LIKIWA LINAINGIA UWANJANI
MUONEKANO WA UWANJA KABLA YA MECHI KUANZA
JUKWAA KUU
No comments:
Post a Comment