Watajwa Hapo Juu ni Wakazi Wa Wilaya ya Mbozi Jimbo la Vwawa.Wamepandishwa Kizimbani Baada Ya Kukaa Mahabusu Kwa Takribani Wiki Tatu Katika Mahabusu Ya Ostarbay-Dar es Salaam Ambapo Wamewasili Leo Vwawa Wakiwa Wamechoka Kutokana na Safari Ndefu na Njaa Kali Kwani Hawakula Tangu Jana.
Akiwasomea Mashitaka Police Prosecutor mnamo majira ya Saa Tisa jioni ya Jana Ya Kwamba Wote Watatu Kwa Nyakati Tofauti Wamehusika na Makosa ya Uchochezi Hivyo Wanashitakiwa Kwa Mujibu wa Sheria za Cyber Crime za Mwaka 2015.Mdude Alisomewa Mashitaka Matatu na Wenzake Shitaka Moja Moja na Wote Wamekana Mashitaka Hayo.
Lakini POLICE PROSECUTOR alisema Dhamana Ipo Wazi.Na Tayari Viongozi Wa Chama Tulijipanga kwa Ajili ya Dhamana Lakini Hakimu Msaidizi wa Mahakama Ya Mwanzo Amezuia Dhamana Kwa Kutoa Sababu Kuwa Yeye Hana Mamlaka ya Kusikiliza Kesi Hio Maana Mwenye Dhamana ni Hakimu Wa Wilaya Ambae Aliondoka Muda Mfupi Kabla Ya Kuingia Mahakamani Kwa Madai Ambayo Hatuyajui na Kumkaimisha Kiti Hakimu wa Mwanzo.
Baada ya Kusomewa Mashitaka Hayo Watuhumiwa Wote Walikana na Walipopewa Nafasi ya Kujitetea Wote Walitoa Sababu Inayofanana Kwamba Wanaomba Dhamana Ili Wapate nafasi Ya Kujitibu Kwani Wakati Wakuhilojiwa Walipigwa Sana Hivyo bado Wanamaumivu Makali Mwilini Maana Hawakutibiwa Ipasavyo.
Wakati Wa Usomaji Wa Kesi Wananchi Hawakuruhisiwa Kuingia Ndani Ya Chumba Cha Mahakama Ambapo Ndani ya Mahakama Alikuwepo Hakimu,Karani,PP pamoja na Askari wengine na Mimi Fanueli Mkisi.Hakimu Aliniinua Na Kunihoji Kama Nina Lolote La kusema Nikamuuliza Kuwa Mhe.Hakimu Ikiwa POLICE PROSECUTOR Amesema Dhamana Iko Wazi Inakuaje Wewe Unaizuia Dhamana?Hakimu Hakunijibu Na Kuahirisha Kesi Mpaka Tarehe 27/09/2016 Lakini Kwa Kuwa Dhamana Ipo Wazikama alivyosema PP Tumepanga Kwenda Kesho(leo) Kuonana na Hakimu wa Wilaya Ili Tufanye Mchakato wa REMOVE ORDER Kabla Ya Tarehe Iliyopangwa
Na FANUEL MKISI -Mwanachama.
DSS TV TUNAWASILISHA TU.
DSS TV TUNAWASILISHA TU.
No comments:
Post a Comment