Thursday, September 1, 2016

Chuo kikuu kilichouza watumwa Washington, Marekani chajutia



Chuo cha Georgetown kiliuza watu 272 ili kulipa madeniImage copyright
Image captionChuo cha Georgetown kiliuza watu 272 ili kulipa madeni
Chuo kikuu kimoja nchini Marekani, ambacho kiliuza watumwa wakati biashara ya utumwa, kimeeleza kujutia kitendo hicho.
Chuo kikuu cha Georgetown, kinachopatikana mjini Washington DC, kimesema kitawapendelea wajukuu wa watumwa waliouzwa na chuo hicho karne ya 19 wakati wa kuwateua wanafunzi wa kujiunga na chuo hicho.
Mwaka 1838, chuo kikuu hicho kiliuza watu 272 ili kuweza kulipa madeni yake.
Waliouzwa walikuwa wanaume, wanawake na watoto.
Tukio hilo lilinakiliwa vyema na kwa sasa watafiti na wachunguzi wamefanikiwa kuwapata baadhi ya jamaa za watumwa waliouzwa.
Miongoni mwa hatua nyingine ambacho chuo hicho kinachukua ni kubadili majina ya majengo yake na kuyapa majina ya watumwa hao.
Aidha, chuo hicho kitafadhili taasisi mpya ya utafiti kuhusu utumwa.

No comments:

Post a Comment