Tuesday, September 13, 2016

BEKI WA PREMIER LEAGUE APATA AJALI MBAYA YA GARI

Beki wa kushoto anayechea katika Ligi Kuu ya England 'Premier League' akiwa ni mchezaji wa timu ya Crystal Palace, Pape Souare amejeruhiwa katika ajali mbaya ya gari alipokuwa katika mitaa ya Jiji la Londo, ambapo ksa sasa yupo hospitali akipata matibabu.

Souare, 26, ameumia kiasi na imeelezwa kuwa atakuwepo hospitalini kwa muda kabla ya kuruhusiwa.






Mchezaji huyo ambaye alikuwemo katika kikosi cha timu yake kilichocheza dhidi ya Middlesbrough, wikiendi iliyopita anaendelea vizuri.

"Klabu inaendelea na mchakato wa kufuatilia kilichotokea, tunawapa pole familia ya Pape pamojana mchezaji mwenyewe,” ilieleza taarifa ya Palace.

Beki huyo raia wa Senegal alitua klabuni hapo akitokea Lille, Januari mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment