Sunday, September 4, 2016

Afcon 2017: Uganda yafuzu mara ya kwanza tangu 1978



Farouk MiyaImage copyright
Image caption

NA KENNEDY SIMUMBA DSS TV,

Uganda imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza katika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1978 baada ya kulaza Comoros Jumapili.
Ushindi wao wa 1-0 uliwawezesha kufuzu kwa fainali zitakazochezewa Gabon mwaka ujao kama mojawapo wa mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili katika makundi.
Wapinzani wao Kundi D Burkina Faso pia walifuzu kwa ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 dhidi ya Botswana, ushindi uliowawezesha kuongoza kundini.
Tunisia na DR Congo pia zilifuzu baada ya kuongoza katika makundi yao.
Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. Waliofuzu ni viongozi wa makundi yote 13, mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili hatua ya makundi, na wenyeji Gabon.
Algeria, Cameroon, Egypt, Ghana, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Mali, Morocco, Senegal na Zimbabwe walijihakikishia nafasi kabla ya mechi za Jumapili.
Katika kufuzu, Uganda pia walifikisha alama 13, kupitia bao la dakika ya 35 la Farouk Miya mjini Kampala, lakini wakaorodheshwa wa pili kwa sababu walilemewa na Burkina Faso klabu hizo mbili zilipokutana.
Mara ya mwisho Uganda kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika ilikuwa miaka 38 iliyopita ambapo walimaliza wa pili baada ya kushindwa fainali an Ghana.

No comments:

Post a Comment