- 19 Agosti 2016
Huu hapa ni mkusanyiko wa picha kutoka Marekani, ambapo vinyago vya utupu vya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump viliwavutia sana wapita njia.
- Vinyago vya utupu vya Donald Trump viliwekwa maeneo mengi ya miji ya New York, Los Angeles, Seattle, San Francisco na Cleveland nchini Marekani mnamo Alhamisi na kuwavutia sana watu.
- Vinyago hivyo vinavyomuonesha Trump akiwa na sura ya ukali viliwekwa chini ya mradi wa INDECLINE, na viliundwa na msanii kutoka Cleveland.
- "Ni kupitia vinyago hivi ambapo tunaonesha umma sura na sifa halisi ya mmoja wa wanasiasa wabaya na wanaochukiwa zaidi Marekani," INDECLINE walisema kupitia taarifa.
- Wapita njia wengi walivutiwa na kufurahishwa na vinyago hivyo, baadhi wakiamua hata kuvibusu...
- ...wengine walijaribu kuiga.
- Kwa jumla, mradi huo ulionekana kuwasisimua sana Wamarekani.
- Lakini wafanyakazi wa bustani na maeneo ya umma New York waliondoa vinyago hivyo. "NYC Parks inapinga vikali kuwekwa kwa vinyago visivyoidhinishwa katika bustani za jiji, bila kujali ukubwa wake," alisema msemaji wa Sam Biederman.
- Maafisa wa kampeni wa Donald Trump kufikia sasa hawajazungumzia vinyago hivyo.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment