Friday, March 2, 2018

MWENYEITI WA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA HATAJA VIKWAZO VINAVYO SABABISHA MADIWANI KUTO KUREJEA HALMASHAURI



Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma MH:ALLY MWAFONGO amezungumzia sababu zinazo sababisha madiwani kutokurejea halmashauri.
Alisema tarehe 26/02/2018 alimuandikia barua mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa tunduma /01/03/18 kuitisha kikao  cha baraza la madiwani tarehe hiyo ni  kuitaji mgogoro wa madiwani na mkuu wa wilaya ya momba MH: JUMA IRANDO unamalizika alisema na sio kumalizika tu bali wao madiwani wanahitaji kuwatumikia wananchi.
Pia anasema anamshukuru waziri wa TAMISEMI MH: SULEIMAN JAPHO alisema kimsingi waziri wa tamisemi alishalimaliza kwa kumtuma naibu waziri alisema alikaa na naibu waziri wakazungumza na naibu waziri kuyachukua kwa ajili ya kuyashughulikia.
Alisema mkuu wa wilaya ya momba MH:JUMA IRANDO alimwambia
kwamba afanye mikutano kwa ajili ya kutengua kauli aliyo isema wakati wa kuondoa ushirikiano na mkuu wa wilaya.
Alisema vikwazo ni kwamba baada ya kutengua kauli na kufuata taratibu zote alimuandikia barua mkurugenzi kwa ajili ya kuitisha kikao tarehe 29 mwezi wa 2 lakini tarehe ilipo fika hapakuwa na maandalizi yoyote kwa ajili ya kikao.